#Local News

MAAFISA WA ZAMANI NYS WAHUKUMIWA KIFUNGO GEREZANI

Aliyekuwa msimamizi wa ununuzi katika idara ya huduma za vijana NYS Hendrick Nyongesa amepata pigo baada ya mahakama kumpa huku ya vifungo viwili vya jumla ya miaka 12 baada ya kupatikana na hatia ya kughushi stakabadhi zilizosababisha kupotea kwa shilingi milioni 791 kati ya mwaka 2014 na 2015.

Nyongesa amehukumiwa Pamoja na aliyekuwa mkurugenzi wa fedha kwenye idara hiyo Samuel Wachenje ambaye amepewa kifungo cha miaka 5 gerezani, wiki moja baada yao kupatikana na hatia hiyo ya ufisadi.

Wawili hao watatumikia vifungo hivyo kwani mahakama haijawapa mwanya wa kulipa faini.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAAFISA WA ZAMANI NYS WAHUKUMIWA KIFUNGO GEREZANI

MAHAKAMA YA RUFAA KUSIKIZA KESI YA GACHAGUA

MAAFISA WA ZAMANI NYS WAHUKUMIWA KIFUNGO GEREZANI

“MUNGU ALINIOKOA NIWAOKOE”- TRUMP

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *