WAHUDUMU WA UHC WAKANA KUWA ‘HEWA’

Utata unaokumba uajiri wa wahudumu wa afya ya wote UHC umechukua mkondo tofauti, wahudumu hao sasa wakipinga madai ya mwenyekiti wa kamati ya afya katika baraza la magavana na ambaye pia ni gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki kwamba kuna wafanyakazi hewa zaidi ya 3,000 miongoni mwao.
Kulingana na wahudumu hao, madai ya gavana huyo ni ukwepaji kutoka kwenye masuala yenye umuhimu, wakisema wako tayari kuhesabiwa.
Aidha, wamesema watahamishiwa tu kwenye serikali za kaunti iwapo watapokezwa barua za uajiri.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa