#Local News

MSIMAMIZI WA BAJETI APINGA OMBI LA SENETA

Msimamizi wa bajeti ya serikali Margaret Nyakang’o amepinga pendekezo la seneta wa Meru Kathuri Murungi la kutaka amzuie gavana Kawira Mwangaza kutoa fedha za kaunti hiyo kwa akaunti zinazomilikiwa na kaunti hiyo, akisema kwamba Mwangaza angali mamlakani.

Kupitia barua iliyoandikwa hapo jana, Nyakang’o amemkumbusha seneta huyo kwamba Mwangaza ana agizo la mahakama linalozuia kutimuliwa kwake kutoka madarakani na hivyo ni ukiukaji wa sheria kukubali ombi lake.

Aidha, Nyakang’o amekariri kwamba Mwangaza atasalia mamlakani hadi mahakama itakapotoa maagizo zaidi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MSIMAMIZI WA BAJETI APINGA OMBI LA SENETA

WAKAZI KITALE WAHANGAIKA, WAKOSOA KeNHA

MSIMAMIZI WA BAJETI APINGA OMBI LA SENETA

EACC YAPONGEZA UAMUZI KUHUSU LENOLKULAL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *