VIJANA 100 WA MAGENGE LIKONI WAJISALIMISHA

Vijana 100 waliokuwa wakijihusisha na uhalifu wamejisalimisha kwa polisi huko Likoni, kaunti ya Mombasa, wakiahidi kuachana na uhalifu.
Kamanda wa Polisi wa Pwani, Ali Nuno, ameahidi kuwasaidia kupata njia mbadala za kujikimu, huku mashirika ya kiraia yakiwasihi kujiunga na vyuo vya TVET vinavyogharamiwa na serikali ya kaunti.
Serikali ya kaunti imeahidi kuwapa ajira wale watakaohitimu.
Imetayarishwa na Janice Marete