AMORIM ANA KIBARUA KIGUMU
Ruben Amorim ndiye kocha wa hivi punde kuingia kwenye kiti moto cha Old Trafford kujaribu kurejesha nyota ya zamani ya Manchester United.
Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ureno ataanza kuinoa klabu hiyo kuanzia Novemba 11 baada ya kumaliza muda wake wa mafanikio katika klabu ya Sporting Lisbon.
Amorim anakuwa kocha wa sita wa kudumu kwa United tangu kocha wa zamani Alex Ferguson kustaafu mwaka wa 2013. Katika miaka 11, United imeshindwa hata kushindana na kushinda Ligi ya Premia au Ligi ya Mabingwa.
Mashetani Wekundu wameanza vibaya zaidi enzi za Ligi Kuu wakiwa na pointi 12 pekee kati ya mechi 10 na kushika nafasi ya 13.
Hata katika mashindano ya daraja la pili la kandanda barani Ulaya, Mashetani Wekundu wanatatizika, bila ushindi katika mechi zao tatu za ufunguzi za Ligi ya Europa.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































