MWANAMME ‘ARUKA’ KUTOKA GHOROFANI NA KUFARIKI
Polisi wanachunguza kisa ambapo mwanamme mmoja ameripotiwa kuruka kutoka ghorofa ya 4 ya jengo moja kwa barabara ya Tom Mboya katikati mwa jiji la Nairobi na kuangukia roshani ya jengo hilo kabla ya kufariki papo hapo.
Imearifiwa kuwa mwanamme huyo alikuwa chumbani na mtu ambaye hadi sasa hajafahamika, na polisi wanachunguza kubaini iwapo ni mauaji au kujitoa uhai.
Kamanda wa polisi wa kituo cha Central Stephen Okal amethibitisha kisa hicho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































