#Local News

RAIS RUTO AFANYA MKUTANO NA WAZIRI MKUU WA HAITI

Rais William Ruto amefanya mkutano waziri mkuu wa Haiti Garry Connley katika ikulu ya Nairobi.

Wawili hao wamejadili swala la kutumwa kwa maafisa zaidi nchini Haiti ili kuimnarisha usalama na kupiga jeki juhudi za kuwakabili magenge ya uhalifu.

Katika kikao na wanahabari Ruto amesema kuwa kuna haja ya polisi wa Kenya kupigwa jeki na maafisa wa mataifa mengine haswa mataifa yaliyostawi.

Ruto aidha amesema kuwa magenge hayo yanaendlewa kukabiliwa na hivi karibuni taifa hilo litakuwa huru.

Ruto aidha amewasifia marais wa mataifa mengine kwa kuunga mkono juhudi za kurejesha amani nchini Haiti

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *