JUNIOR STARLETS YAICHAPA UGANDA 3-0

Timu ya taifa ya wasichana U-17 Junior Starlets imeicharaza Uganda 3-0 katika Uwanja wa Nyayo, ikifuzu kwa raundi ya tatu ya kufuzu Kombe la Dunia la FIFA U-17.
Brenda Achieng alifunga mabao mawili, huku Patience Asiko akipachika moja mapema dakika ya 4. Ushindi huu unakamilisha jumla ya 5-0 kwa mechi zote mbili baada ya ushindi wa 2-0 jijini
Kampala wiki iliyopita.
Kocha Mildred Cheche alisifu juhudi za timu, huku nahodha Halima Imbachi akielezea utayari wao wa kukabiliana na Cameroon katika raundi inayofuata.
Imetayarishwa na Janice Marete