#uncategorized

RATIBA YA RAIS RUTO ANAPOANZA ZIARA YA KISERIKALI YA SIKU 4 NCHINI MAREKANI

Rais William Ruto anatarajiwa kuwasili nchini marekani kuanza rasmi ziara yake ya siku nne nchini humo , hii ni kufuatia mwaliko wa rais wa marekani Joe Biden

Msemaji wa ikulu Hussein Mohamed akitoa ratiba hiyo amesema hii leo rais Ruto atakuwa katika jimbo la Atlanta Georgia ambapo atatembelea Maktaba ya Rais ya Carter na Makavazi. Ambapo ataangazia kujitolea kwa mataifa haya mawili katika maswala ya uongozi na kukabili ufisadi kabla ya kutembelea Kanisa la Ebenezer Baptist kutoa heshima kwa mapambano ya Haki za Kiraia na kusisitiza jinsi dini inaweza kuwa na nguvu ya wema.

keshoJumanne, Rais Ruto atakuwa katika Chuo cha Spelman ambapo atajadili jukumu muhimu la elimu ya juu, haswa sayansi na teknolojia katika kuimarisha maendeleo .

Kisha baadae atatembelea katika Studio za Tyler Perry kabla ya kutembelea makao makuu ya Coca-Cola, ambapo ushirikiano mpya wa uwekezaji utaangaziwa.

Kabla ya  kuzindua chapa ya mitindo ya reja reja ya Kenya, duka la kwanza la Vivo nchini Marekani.

Imetayarishwa na: Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *