#Local News

SABA SABA YAVUNJA HISTORIA

Maandamano ya kuadhimisha siku ya Saba Saba yametangazwa kuwa yenye maafa makubwa zaidi kuwahi kutokea katika maandamano humu nchini, idadi ya waliouawa ikipanda hadi watu 32.

Kulingana na mashiirika ya kutetea haki za kibinadamu ikiwemo tume ya KNHCR, jumla ya watu 115 wameuawa kwenye maandamano kati ya Juni mwaka jana hadi sasa, familia katika maeneo ya Kiseria, Ngong na Kutus zikiwa miongoni mwa wanaoomboleza vifo kutokana na maandamano ya Saba Saba.

Upasuaji wa maiti umeonyesha vifo hivyo vilisababishwa na majeraha ya risasi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SABA SABA YAVUNJA HISTORIA

NYAMBUA LENGO LAKE NI KUSHINDA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *