THURAM AJIUNGA NA JUVENTUS
Kiungo wa kati wa Ufaransa Khephren Thuram amejiunga na Juventus kutoka klabu ya Nice ya Ligue 1 kwa mkataba wa miaka mitano wa euro milioni 20.
Thuram, 23, anafuata nyayo za baba yake, Lilian, beki wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa aliyeichezea Juventus kuanzia 2001 hadi 2006.
Khephren Thuram, ambaye alizaliwa nchini Italia wakati baba yake akiwa Parma, ameichezea Ufaransa mechi moja ya kimataifa na kabla ya kuingia Nice – alikuwa Monaco.
Thuram alikuwa tayari kuchezea wenyeji Ufaransa katika mashindano ya soka ya Michezo ya Olimpiki ya Paris chini ya kocha Thierry Henry lakini Juventus hawakuwa na nia ya kusajili mchezaji wao mpya kushiriki Michezo hiyo, na kusababisha kuondoka kwake kutoka kwa timu ya Ufaransa.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































