#Business

KAMISHNA MKUU WA KRA AHIMIZA NCHI ZA AFRIKA KUBORESHA UKUSANYAJI WA USHURU

Kamishna Mkuu wa kampuni ya ukusanyaji ushuru nchini KRA Humphrey Wattanga amezitaka nchi za Afrika kuboresha vitengo vya usimamizi  wa ushuru na ukusanyaji wa mapato licha ya upungufu katika sekta ya uongozi na mtiririko wa fedha haramu.

Wattanga ametoa wito huo wakati wa mkutano ambao umeleta pamoja wataalam wa ushuru kujadili mikakati ya kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kupitia hatua madhubuti za ushuru barani Afrika.

Kongamano la siku tatu la 9 lililohudhuriwa na maafisa wa bodi ya ukusanjyaji wa Kodi barani Afrika mwaka 2024 limeleta pamoja zaidi ya wajumbe 200, wakiwemo wasimamizi wa ushuru wa Afrika na washirika wa maendeleo, kushughulikia maswala muhimu ya kodi kama vile mapato kutokana na biashara ya mipakani.

Vile vile ametoa wito kwa tawala za ushuru za Kiafrika kulinda haki za walipa kodi, kuzingatia uadilifu, haki, na uwajibikaji wakati wa kuwahudumia, na kutoa hudumai ya mifumo madhubuti ya kutatua migogoro.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi.

KAMISHNA MKUU WA KRA AHIMIZA NCHI ZA AFRIKA KUBORESHA UKUSANYAJI WA USHURU

MENEJA WA NGCDF MASHAKANI

KAMISHNA MKUU WA KRA AHIMIZA NCHI ZA AFRIKA KUBORESHA UKUSANYAJI WA USHURU

WATU ZAIDI YA MILIONI 74 WAKABILIWA NA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *