TUKO PABAYA KIFEDHA, SRC

Mwenyekiti wa tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi wa umma SRC Lynn Mengich ameibua hofu kuhusiana na kiwango cha juu cha fedha zinazotumiwa katika kulipa mishahara, ambacho kwa sasa ni asilimia 43 ya mapato ya serikali.
Akizungumza na wanahabari, Mengich amesema matumizi ya fedha za serikali yamekuwa yakiongezeka licha ya juhudi za serikali kubana matumizi.
Aidha, amesema matumizi hayo ambayo yamezidi shilingi trilioni moja, pia yamezidi kiwango cha asilimia 35 kinyume na sheria za usimamizi wa fedha za umma.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa