SERIKALI YATOA BILIONI 18 ZA KUJENGA MADARASA YA GREDI 9
Juhudi za ujenzi wa madarasa 16,000 kwa wanafunzi wa gredi ya 9 ambao wanaanza masomo yao mwaka ujao zimepigwa jeki baada ya serikali kutoa shilingi bilioni 18.8 za kuwezesha ujenzi huo.
Akithibitisha kutolewa kwa fedha hizo, Waziri wa Elimu Julius Ogamba ametoa hakikisho kwamba serikali imejitolea kuhakikisha kuwa madarasa hayo yanakamilika kwa wakati ili kufanikisha masomo hayo.
Ameongeza kuwa wanashirikiana na hazina ya NG-CDF, hazina hiyo ikipewa jukumu la kujenga madarasa 5,000 huku yaliyosalia yakijengwa na wizara ya elimu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































