MBUNGE OCHIENG’ ATISHIA KUWASILISHA HOJA YA KUMTIMUA MASENGELI IWAPO HATAJIUZULU LEO

Mbunge wa Ugenya kaunti ya Siaya David Ochieng’ ametishia kuwasilisha hoja katika Bunge la Kitaifa ya kumtimua kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli iwapo atakosa kujiuzulu hii leo.
Kwa maoni ya Ochieng, Masengeli amethibitika kuwa mtu mhuni na hawezi kuaminiwa na jukumu muhimu la kusimamia jeshi la polisi la Kenya na kulinda raia na kwamba iwapo Masengeli atashindwa kuondoka madarakani kwa hiari yake ataanzisha hoja ya kumwondoa katika Bunge hilo ili kulazimisha kuondoka kwake.
Imetayarishwa na Janice Marete