DUALE AKANA KUWAATISHIA WANAJESHI
Waziri mteule wa mazingira Aden Duale amepinga madai kwamba maafisa wakuu wa jeshi la ulinzi KDF walikuwa wakimwogopa alipokuwa Waziri wa ulinzi, na badala yake amesema kwamba huenda waliogopa mtindo wake wa uongozi.
Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya uteuzi kubaini uwezo wake kwenye wizara mpya, Duale amesema mtindo wake wa uongozi umekuwa ule ule tangu alipokuwa kiongozi katika bunge la kitaifa.
Aidha, Duale amesema yuko tayari kuiendesha wizara ya mazingira na mabadiliko ya hali ya anga, huku akiulaumu usimamizi wa kaunti ya Nairobi kutokana na uchafuzi wa mazingira.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































