ODINGA AWAKOSOA WABUNGE KUHUSU MASAIBU YA KAUNTI
Huku kukishuhudiwa mtafaruku baina ya bunge la kitaifa na lile la seneti kuhusu mgao wa serikali za kaunti ambao umelemaza utoaji huduma mashinani, waziri mkuu wa zamani Raila Odinga amelishutumu bunge la kitaifa kutokana na mahangaiko hayo.
Katika kikao na wanahabari jijini Nairobi, Odinga amesema kupunguzwa kwa mgao huo kutoka shilingi bilioni 400 hadi bilioni 380 kutatatiza shughuli za serikali hizo.
Aidha, ameshutumu vikali hatua ya bunge la kitaifa kuwasilisha mswada unaotaka wapewe sehemu ya usimamizi wa mgao wa serikali za kaunti.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































