NITALETA MEDALI NYUMBANI

Zeddy Cherotich Amekiri Kwamba Yuko Chini Ya Shinikizo La Kutwaa Medali Ya Kwanza Ya Kenya Katika Mchezo Wa Judo, Kitengo Cha Wanawake Katika Michezo Ya Olimpiki Jijini Paris, Ufaransa.
Mwana Judo Huyo Wa Kikosi Cha KDF, Ambaye Pia Alishiriki Mashindano Ya Dunia Huko Abu Dhabi Kabla Ya Kufuzu Kwa Michezo Ya Olimpiki, Alitua Jijini Miramas Jumapili Ambapo Amekuwa Akifanya Mazoezi Kabla Ya Kuelekea Paris Kwa Michezo Hiyo Inayotarajiwa Kuanza Rasmi Kesho Kutwa 26 Hadi 11 Agosti, 2024.
Mchezaji Huyo Mwenye Umri Wa Miaka 34 Alijipatia Nafasi Yake Katika Kitengo Cha Uzani Wa Juu Cha Judo Katika Makala Haya Baada Ya Kujikusanyia Pointi 384 Katika Mchujo Wa Afrika, Na Atakuwa Miongoni Mwa Wanawake 12 Kutoka Afrika Watakaoshiriki Fani Hiyo.
Cherotich Yuko Chini Ya Ukufunzi Wa Makocha David Busolo Na Mjapani Assura Yosuke, Ambaye Anamfundisha Kupitia Kwa Msaada Wa Shirikisho La Judo Duniani IGF.
Imetayarishwa na Nelson Andati