RUTO KUWARUDISHA VIJANA ‘MITAANI’

Rais William Ruto ametangaza kurejeshwa kwa mpango wa kazi mtaani ulioanzishwa na mtangulizi wake Uhuru Kenyatta kabla ya Ruto kuusimamisha punde alipoingia mamlakani kwa kisingizio kwamba ulikuwa ukitumika kufuja fedha za umma.
Akizungumza katika kaunti ya Nakuru, Ruto amesema serikali yake imeweka mikakati ya kuongeza raslimali za kuongeza kazi kwa vijana.
Aidha, Rais amesema kuwa serikali yake imemua kusikiliza sauti za wananchi ili kutoa huduma stahili kwa wananchi.
Wakati uo huo, Rais Ruto amewaonya anaowaita wafadhili wa vurugu hapa nchini, akiwataka Wakenya kudumisha amani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa