TUACHE KUTUMIA PESA YA UMMA VIBAYA; MARGARET NYAKANGO

Mdhibiti wa bajeti Margaret Nyakango ameilaumu idara za umma kwa kutumia asilimia kubwa za fedha zilizotengewa miradi ya maendeleo kwa ziara za humu nchini na mataifa ya nje ya nchi
Kulingana na nyakango serikali imetumia shilingi bilioni 18.18 kwa zira katika mwaka wa kifedha 2023-2024.
Kwa mujibu wa ripoti ya nyakango idara 35 ikiwemo ofisi ya rais na ofisi ya naibu wake zimekuwa zikitumia fedha kwa shughuli mbali mbali bila kuwasilisha ripoti ya matumizi ya fedha hizo kwa ofisi ya mdhibiti wa bajeti.
Nyakango vile vile ameongeza kuwa kuna ubathirifu wa fedha katika matumizi hayo katika sekta ya umma na kukinzana na ahadi yar ais kwamba serikali yake itabana matumizi ya fedha katika juhudi za kufufua uchumi.
Imetayarishwa na Janice Marete