WAKAZI WA, SUNA MASHARIKI, WALALAMIKIA ONGEZEKO LA UHALIFU
Wakazi wa Kakrao, Suna Mashariki, kaunti ya Migori, wamelalamikia kuongezeka kwa visa vya uhalifu, huku Kaimu Chifu Wyckliff Onyango akisema zaidi ya watu 30 wameshambuliwa na kundi la vijana wasiojulikana.
Wikiendi iliyopita pekee, watu kumi walilengwa, lakini washambuliaji hawaibi, hivyo nia yao haijulikani. Onyango ametoa wito wa ushirikiano kati ya wakazi na vyombo vya usalama ili kudhibiti genge hilo.
Wakazi wanataka kituo cha polisi eneo hilo, wakidai polisi wanakosa magari ya doria na kushindwa kuitikia msaada kwa wakati.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































