MAANDALIZI YA MITIHANI TAYARI, KNEC

Watahiniwa 2,279,414 ndio watakaokalia mitihani ya kitaifa yam waka huu, baraza la mitihani ya kitaifa KNEC likitoa hakikisho kwamba zoezi hilo litaendeshwa kwa njia ifaayo.
Kwa mujibu wa KNEC, mitihani ya kidato cha 4 KCSE itafanyika katika vituo 10,565, huku watahiniwa 1,303, 913 wa KPSEA wakiratibiwa kufanya mitihani yao katika vituo 35,573 kote nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu wa mitihani yam waka huu, afisa mkuu mtendaji wa KNEC David Njegere, amesema kwamba usalama wa karatasi za mitihani umehakikishwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa