WABUNGE KUPINGA KUPOKONYWA DONGE LA NG-CDF

Wabunge wameapa kuwasilisha kesi katika mahakama ya rufaa kupinga uamuzi wa makamama kuu ulioharamisha sheria ya hazina ya kustawisha maeneo bunge NG-CDF, wakishikilia kwamba hazina hiyo imewanufaisha wakazi wa maeneo ya mashinani.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa ambaye pia ni mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro, wabunge wameitaka idara ya mahakama kusikiliza maoni ya wakenya kuhusiana na sheria hiyo.
Hata hivyo, walalamishi kwenye kesi hiyo wamepongeza uamuzi wa mahakama, wakiwataka wabunge kuangazia majukumu yao ya kikatiba.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa