MK CHAUNDA UPINZANI ‘KUKABILI’ SERIKALI

Chama cha Umkhonto we Sizwe (MK) cha kinachoongozwa na rais wa zamani Jacob Zuma nchini Afrika Kusini, kimetangaza kuungana na vyama vingine vya upinzani kwa lengo la kuikabili serikali iliyoundwa na vyama vya ANC na DA kwenye uchaguzi wa hivi punde.
Haya yanajiri baada ya ANC na DA kuungana na kubuni serikali ambayo wameiitaja kuwa ya umoja wa kitaifa.
Chama cha Umukhonto we sizwe kiliwanshangaza wengi na kumaliza katika nafasi ya tatu kikiwa na wabunge 58 kati ya 400, hatua iliyosababisha ANC kupoteza nafasi ya viongozi walio wengi katika bunge nchini humo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa