WAKAZI WA TRANSNZOIA WAHIMIZWA KUKUMBATIA MPANGO WA USALAMA

Wakazi wa eneo la Namanjalala moi farm kata ya Waitaluk kaunti ya Transnzolia wamehimizwa kuendelea kukumbatia mpango wa usalama ambao kulingana na wakazi utasaidia kudumisha amani na kukabiliana na utovu wa usalama katika eneo hilo.
Katika kikao na wanahabari baada ya zoezi la kushirikisha umma kutekeleza wajibu wao kikatiba kuwachagua viongozi wao.
Mwenyekiti wa mpango huo John Tudula anasema kuwa kila mwanafamilia ana jukumu la kumjua mwenzake ili kuziba mianya ya wahalifu kujificha miongoni mwao kama njia mojawapo ya kujonyesha uzalendo.
Imetayarishwa na Janice Marete