#Local News

MTU MMOJA AFARIKI KATIKA MLIPUKO WA GESI KATIKA KAUNTI YA HOMABAY

Mwanaume wa makamo amefariki na mwingine kujeruhiwa katika mlipuko wa gesi uliotokea Oyugis, Rachuonyo Kusini, Kaunti ya Homa Bay.

Mwanaume huyo, ambaye bado hajafahamika, amefariki papo hapo baada ya kulipukiwa na mtungi wa gesi.

Chifu wa Oyugis, Emily Owuor, amesema mwathiriwa huyo alikuwa amesimama takriban mita 20 kutoka eneo la mlipuko alipogongwa na vipande vya mtungi wa gesi.

Mwanaume mwingine amejeruhiwa vibaya kwenye tukio hilo na kukimbizwa katika Hospitali kwa matibabu.

Baadaye aliachiliwa hospitalini baada ya kupatiwa matibabu. Mlipuko huo ulitokea kwenye duka la muuzaji wa mitungi ya gesi.

Kamanda wa polisi wa Rachuonyo Kusini, Philemon Saera, amesema moto huo ulianza katika duka la kinyozi jirani kabla ya kusambaa kwenye duka lililokuwa na mitungi ya gesi na mali nyingine.

Imetayarishwa na Janice Marete

MTU MMOJA AFARIKI KATIKA MLIPUKO WA GESI KATIKA KAUNTI YA HOMABAY

JE MWANGA WA MWANGAZA UTAZIMWA?

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *