#Sports

OBILO AFURAHISHWA NA USHINDI WA KIKOSI CHAKE

Kocha mkuu wa Zetech Sparks Maurice Obilo amefurahishwa na ushindi wa wasichana wake mara mbili wikendi katika mechi ya ligi iliyoandaliwa katika uwanja wa Nyayo Gymnasium, Nairobi licha ya kukosa mazoezi ya kutosha wiki jana.

Cheche waliwachapa wapinzani wao wa vyuo vikuu USIU Flames 65-60 siku ya Jumamosi kabla ya kuwafunga African Nazarene University (ANU Panthers) 57-43 siku ya Jumapili ili kuendeleza mwendo wao mzuri katika ligi kuu ya kitaifa ya mpira wa vikapu ya wanawake.

Mchezo wa Jumapili dhidi ya ANU Panthers, Zetech walianza vyema kwa kushinda robo ya kwanza 14-10 kabla ya kupoteza kidogo robo ya pili 08-07 kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 21-18.

Walidai robo ya tatu 13-09 kabla ya Zetech kuibuka kidedea katika robo ya mwisho na kushinda 27-12 mchezo ulimalizika kwa 57-43 kwa kishindo cha mwisho.

Wanafunzi hao sasa wamefikisha pointi 28 katika michezo 15, wakishinda 13 na kupoteza miwili pekee

Imetayrishwa na Nelson Andati

OBILO AFURAHISHWA NA USHINDI WA KIKOSI CHAKE

MAHAKAMA YAHARAMISHA KARO YA ZIADA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *