KARIOBANGI SHARKS WAREJEA KWA KISHINDO KPL
Ligi kuu ya soka nchini FKF premier ligi imeshuhudia mechi kadhaa mwishoni mwa juma, mechi za jana zikihusisha Shabana FC na Ulinzi Stars ambao walitoka sare ya mabao 2, katika uwanja wa Ulinzi sports complex.
Hata hivyo, patashika ilishuhudiwa wakati wa mechi hiyo ambapo mashabiki waliharibu mali kadhaa uwanjani na kusababisha majeruhi kwa watu kadhaa.
Matokeo sawa yaliandikishwa na Tusker dhidi ya Home Boyz, nayo Kariobangi sharks ambayo imerejea ligini baada ya kukesha kwenye kijibaridi cha National Super League msimu jana, ikichapa Murang’a Seals 3:0
Baada ya mechi 3, KCB wanaongoza ligi kwa alama 7 sawa na kariobangi Sharks, AFC Leopards ni 3 kwa alama 6, alama saw ana limbukeni Mara Sugar ambao wako katika nafgasi ya 4.
Mabingwa watetezi Gor Mahi ana Kenya Police bado hawajacheza mechi ya ligi kutokana na kibarua cha bara.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































