RUTO AFUNGUA NJIA KWA IEBC
Rais William Ruto ametia saini mswada wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuwa sheria, na hivyo kutoa nafasi kwa kubuniwa kwa jopo la uteuzi wa makamishna wapya wa tume hiyo.
Hafla hiyo imeandaliwa katika jumba la mikutano KICC, Rais akiwa ameandamana na Naibu wake Rigathi Gachagua, aliyekuwa Waziri mkuu Raila Odinga na makamu wa rais wa zamani kalonzo Msuyoka.
Akiidhinisha mswada huo ambao ni wa kwanza kupitishwa na bunge kufuatia mapendekezo ya ripoti ya NADCO, Rais Ruto ameutaja mswada huo kuwa kama “ushuhuda kwamba kenya inaweza kustahimili hali ngumu.”
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































