IKULU NA AFISI YA NAIBU RAIS KUATHIRIKA ZAIDI KUFUATIA KUITHINISHWA KWA MSWADA WA ZIADA

Ikulu na afisi ya Naibu wa Rais zimesalia kuwa afisi zilizoathiriwa zaidi kufuatia kuidhinishwa kwa Mswada wa Uidhinishaji wa Ziada yaani suplementary budget (Na.2) wa 2024.
Mswada uliopitishwa wiki jana unalenga kurekebisha mgao wa bajeti kwa mihimili mitatu ya serikali ili kushughulikia upungufu wa mapato wa Shilingi bilioni 344 kufuatia kukataliwa kwa Mswada wa Fedha wa 2024.
Itashuhudia afisi zote mbili zikipoteza Shilingi bilioni 6 huku Hazina pia ikiwa na punguzo kubwa la Shilingi bilioni 7
Imetayarishwa na Janice Marete