MCHEZAJI BARNABAS OWUOR KUAGANA NA STRATHMORE LEOS

Barnabas Owuor, mchezaji wa Strathmore Leos, ametangaza kuwa msimu huu utakuwa wa mwisho kwake kuichezea timu hiyo baada ya kuhudumu kwa zaidi ya miaka kumi.
Tangazo hilo linahitimisha kipindi cha dhahabu kwa mmoja wa wachezaji wenye ushawishi mkubwa katika timu hiyo ya chuo kikuu.
Safari yake ya mchezo wa raga ilianza katika Shule ya Upili ya Dagoretti, kisha akaichezea Mwamba RFC kabla ya kupata ufadhili wa masomo katika Chuo Kikuu cha Strathmore.
Amesema ni kipindi kigumu kuondoka katika timu ambayo imekuwa nyumbani kwake kwa muongo mmoja.
Imetayarishwa na Janice Marete