MUDAVADI: KENYA, UCHINA KUSHIKAMANA ZAIDI

Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi amesema kwamba serikali ya Kenya inalenga kuboresha uwekezaji kati yake na Uchina kwa lengo la kuimarisha biashara na mshikamano baina ya mataifa hayo mawili. Akizungumza katika ubalozi wa taifa hilo jijini Nairobi, Mudavadi amesema kwamba hatua za uwekezaji na ushiriikiano kwenye miradi mbali mbali umesaidia kenya kupiga hatua za kimaendeleo, […]

GACHAGUA APATA PIGO MAHAKAMANI, HOJA DHIDI YAKE KUENDELEA

Naibu rais Rigathi Gachagua amepata pigo baada ya mahakama kudinda kuzuia bunge kusitisha mchakato wa kumbandua kutoka afisini. Kesi hiyo imewasilishwa na aliyekuwa seneta wa Kakamega Cleophas Malala, akitaka mahakama izuie kuwasilishwa bungeni na kujadiliwa kwa mswada huo kwa misingi kwamba bunge la kitaifa na lile la seneti hayajaafikia usawa wa kijinsia kuendesha kikao hicho. […]

PVK YAITAKA SERIKALI KUWAJIBIKIA WAKENYA

Viongozi wa kidini wa Pentecostal Voice Of Kenya wamejitokeza kukashifu machafuko ya kisiasa yanaoendele humu nchini haswa suwala la kubanduliwa mamlakani kwa naibu wa rais Rigathi Gachagua Wakiongozwa na mwenyekiti wao Apostal Peter Manyuru ambaye pia ni mwazilishi wa kanisa la Jesus Teaching Ministry JTM wamesema kuwa huenda serikali ina njama ya kuwafumba macho wananchi […]

ODPP KUWASHTAKI WANDANI, WASAIDIZI WA GACHAGUA

Wakenya sasa wanasubiri kuona ni lini wandani na wasaidizi wa naibu rais Rigathi Gachagua wakiwemo wabunge wawili, watakamatwa na kufikishwa mahakamani kufunguliwa mashtaka ya kupanga njama ya kutekeleza uhalifu na utakatishaji wa fedha yaani money laundering. Hii ni baada ya afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma ODPP kukubali pendekezo ya la idara ya upelelezi […]

NI UONGO, WANAHARAKATI WAMJIBU KINDIKI

Vuta nikuvute inaendelea baina ya serikali na wanaharakati kuhusiana na lengo la maandamano ya kizazi cha Gen Z yaliyoshuhudiwa nchini katika mwezi wa Juni na Julai mwaka huu, wanaharakati sasa wakipinga madai ya waziri wa usalama Kithure Kindiki kwamba walikuwa na lengo la kupindua serikali kupitia mandamano hayo. Katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga […]

CHIFU ATAKA KITUO CHA POLISI KUKABILI WIZI

Wakazi katika eneo la Ngweso kaunti ya Homa Bay wakiongozwa na chifu wa eneo hilo sasa wanaitaka serikali kujenga kituo cha polisi eneo hilo ili kukabili visa vya wizi hasa unaoelenga pikipiki kila siku ya soko. Aidha, wamewataka polisi kuimarisha doria ili kukomesha visa hivyo ambavyo vimekithiri. Wakazi hao wameyasema haya baada ya kumpiga hadi […]

RUTO AKOSOA MFUMO WA UN, AU

Rais William Ruto amekariri kujitolea kwa serikali yake katika kurejesha utulivu nchini Haiti, akiahidi kuwatuma polisi zaidi nchini humo ili kufikisha jumla ya polisi 2,500 kufikia Januari mwaka ujao. Akizungumza katika kongamano la umoja wa mataifa UN nchini Marekani, Ruto ametetea hatua hiyo na kuwapongeza polisi wa Kenya kutokana na umahiri wao wa kukabili magenge […]

KIFO CHA KIPTUM KILICHUKUA NYOTA MKUBWA

Rais wa shirikisho la Riadha Duniani Sebastien Coe amesema kifo cha kusikitisha cha Kelvin Kiptum na rekodi yake kuu ya dunia ilikuwa muhimu katika kumtunuku zawadi maalum mbio za Chicago Marathon (1977) katika kitengo cha mashindano hayo. Kiptum, ambaye alifariki katika ajali ya barabarani mapema mwaka huu, alivunja rekodi ya dunia ya mbio za marathon […]

LUANDA VILLA IKO KWA NAFASI NZURI MSIMU HUU

Kocha wa Luanda Villa Gilbert Selebwa ana imani kwamba kikosi chake kimejitayarisha vilivyo kukabiliana na 3KFC ya Embu na kuibuka washindi katika mechi yao ya pili ya ligi Ya kitaifa DARAJA LA PILI NSL iliyoratibiwa Jumapili hii. Selebwa anasema ushindi dhidi ya timu bora zaidi Kibera Blackstars ni dhihirisho kwamba anaweza kuandikisha ushindi wake wa […]

UCHAGUZI WA FKF WAPANGWA TAREHE SABA DISEMBA

Bodi ya Uchaguzi ya FKF imepanga tarehe 7 Disemba kuwa tarehe ambayo kura za urais zitafanyika katika kile ambacho kitakuwa kilele cha mchakato ambao umekuwa na panda shuka nyingi kwa miezi kadhaa. Kwa mujibu taratibu za kuelekea uchuaguzi huo iliyotolewa na Bodi hiyo ya Uchaguzi hii leo, Kamati ya Utendaji ya kitaifa na wawaniaji urais […]