WAFANYABIASHARA WAKADIRIA HASARA YA MAANDAMANO
Baada ya kupata nafuu kutokana na maandamano ya wiki jana ya Gen Z, wafanyabiashara wengi sasa wanahesabu hasara kufuatia maandamano ya hapo jana ambayo yalifanyika katika zaidi ya kaunti 25.
Wafanyabiashara ambao wamezungumza na vyombo vya habari wamesema kuwa baadhi ya maduka yao yaliharibiwa na mali kuibiwa baada ya maandamano hayo, ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa ya amani asubuhi, na baadaye kugeuka kuwa ya fujo na baada ya muda mfupi yalipenyezwa na waharibifu.
Miongoni mwa kaunti zilizoathirika zaidi ni Nairobi, Nakuru, Uasin Gishu, Nyeri, Embu, Taita Taveta, na Busia. Kiwango kamili cha hasara hiyo bado hakijathibitishwa, lakini wataalam wanakadiria kuwa inaweza kufikia mabilioni ya shilingi za Kenya.
Jijini Nairobi, barabara ya Moi Avenue ndiyo iliyoathirika zaidi, huku maduka kadhaa yakivunjwa, na kuacha nyuma eneo la vioo vilivyovunjwa na mali iliyoharibika.
Imetayrishwa na Maureen Amwai
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































