#Local News

EACC YAREJESHA ARDHI YA UMMA

Tume ya kukabili ufisadi EACC imefaulu kurejesha vipande 12 vya ardhi ya umma iliyokuwa imenyakuliwa katika kaunti za Kakamega, Bungoma na Busia.

Akizungumza huko Mumias meneja wa EACC tawi la magharibi Eric Ngumbi anasema ardhi hizo zilichukuliwa na watu binafsi wakishirikiana na wafanyikazi wa serikali.

Anasema kwa sasa wanafuatilia vipande vingine 56 vinavyoaminika kutwaliwa na vinavyomilikiwa na idara tofauti za serikali ikiwemo ile ya makaazi mahakama na mamlaka ya viwanja vya ndege.

Imetayrishwa na Antony Nyonesa

EACC YAREJESHA ARDHI YA UMMA

KINDIKI ASIFIA E-CITIZEN

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *