NSL: FORTUNE SACCO YAPANDA JUU, MAKALI YA MOMBASA UNITED YA NZOIA

Fortune Sacco ilisonga mbele kwenye jedwali la Ligi Kuu ya Kitaifa (NSL) baada ya kulaza Darajani Gogo 1-0 Uwanja wa Vipor huku Naivas FC ikitoka sare ya 1-1 na 3K FC Uwanja wa Moi Kisumu Jana Jumapili.
Elias Mugane alifunga dakika za lala salama na kusaidia Fortune kuruka 3K FC katika kilele cha ligi ya daraja la pili na kwa sasa wanaongoza ligi hiyo ya timu 20 kwa alama 11, sawa na wapya ligi lakini timu hiyo yenye makao yake Kaunti ya Kirinyaga inajivunia tofauti ya mabao ya juu zaidi.
Huko Serani Sports Ground, Mombasa United iliishinda Nzoia Sugar inayotatizika 1-0 huku wenyeji wa pwani wakiambulia ushindi wa tatu wa NSL msimu huu katika uwanja wa Serani Sports Ground mjini Mombasa.
Imetayarishwa na Janice Marete