#Local News

BII KUMTANGAZA NAIBU MPYA ‘MARA MOJA’

Gavana wa Uasin Gishu Jonathan Bii amesema kwamba atamtangaza naibu wake mpya hivi karibuni baada ya naibu wake John Barorot kujiuzulu, akisema amepata kazi katika shirika moja la kimataifa.

Kwa mujibu wa Bii, atamteua mtu mwenye uwezo saw ana ule wa Barorot na kuwasilisha jina lake kwa bunge la kaunti ya Uasin Gishu kwa uidhinishaji.

Duru zimearifu kwamba miongoni mwa wanaotarajiwa kuteuliwa ni aliyekuwa mbunge wa Moiben Sila Tiren, mwakilishi wadi wa zamani Pius Kigen, Mhandisi Anthony Chelimo na Waziri wa biashara kwenye kaunti hiyo Martha Cheruto.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *