DUALE AIMBA WIMBO WA RAIS RUTO
Waziri wa afya Aden Duale amekariri kauli ya Rais William Ruto kwamba utawala wa Kenya Kwanza hautaruhusu vitisho kutoka kwa wapinzani wake, akisema mambo sasa yatachukua mkondo tofauti kuenda mbele.
Katikia mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini, Duale ametetea kauli ya Rais Ruto ya kuwataka polisi kuwafyetulia risasi miguuni wanaovamia mali wakati wa maandamano.
Duale amesema matukio hayo ni kigaidi na wahusika watakabiliwa kisheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































