RUUD AVUNA USHINDI KAMA KAIMU MENEJA

Ruud Van Nistelrooy alianza kwa ushindi kama meneja wa muda wa Manchester United kwa kuifunga Leicester 5-2 na kuingia robo-fainali ya Kombe la Ligi siku ya Jumatano
Arsenal na Liverpool walikuwa miongoni mwa timu nyingine zilizojikatia tiketi ya kucheza nane bora, lakini Chelsea walichapwa 2-0 na Newcastle.
Gwiji wa United akiwa mchezaji, Ruud Van alisisitizwa kushika nafasi ya bosi wa muda baada ya Mashetani Wekundu kumfukuza Erik ten Hag Jumatatu kufuatia mwanzo mbaya wa msimu.
Kulingana na ripoti kutoka Ureno, Amorim atasalia Sporting kwa mechi tatu zijazo kabla ya kukamilisha uhamisho wake wakati wa mapumziko ya kimataifa ya Novemba.
Imetayarishwa na Nelson Andati