NAKHUMICHA ASEMA MSWADA UMEATHIRI SHIF

Waziri wa afya Susan Nakhumicha ametangaza kwamba wakenya watakuwa na uwezo wa kujisajili katika mpango wa afya ya jamii SHIF kuanzia tarehe 1 Julai kupitia tovuti ya mamlaka ya afya ya kijamii. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Nakhumicha amesema wizara yake inafanya marekebisho kuhusiana na hazina mbali mbali za afya ikiwemo ile ya matibabu […]

WANDAYI: TEKELEZA NADCO KABLA TUONGEE

Kiongozi wa walio wachache katika bunge la kiataifa Opiyo Wandayi amemtaka rais william Ruto kutekeleza ripoti ya kamati ya mazungumzo ya kitaifa NADCO kabla ya mazungumzo zaidi kufanyika. Wandayi amesema kwamba muungano wa Azimio unaamini kwamba mazungumzo yanfaa kwa taifa ila utekelezaji wa ripoti hiyo utaashiria kujitolea kwa rais ruto kufanya mazungumzo kwa nia njema. […]

GACHAGUA KIZIMBANI?

Mwanaharakati kwa jina Frederick Bikeri amemshtaki Naibu Rais Rigathi gachagua mahakamani kuhusiana na matamshi ya Gachagua dhidi ya mkurugenzi wa idara ya ujasusi NIS Noordin Haji. Kulingana na mwanaharakati huyo, matamshi ya Gachagua dhidi ya Haji hayana ukweli, yenye uchochezi na kinyume na sheria, na kwamba hayaambatani na viwango vya mienendo ya mtumishi wa umma […]

HAZINA YA KITAIFA NJIA PANDA

Hazina ya kitaifa sasa inakabiliwa na hali ngumu ya kusawazisha matumizi ya nchi kwa mwaka ujao wa kifedha unaoanza wiki ijayo, kufuatia kuondolewa kwa Mswada wa Fedha wa 2024 wenye utata. Uamuzi wa Rais William Ruto siku ya Jumatano kudinda kuidhinisha mswada huo kufuatia maandamano unaiacha Hazina ya kitaifa na pengo la shilingi bilioni 302 […]

SERIKALI KUIMARISHA EPZ

Serikali inafanya mazungumzo ya kuweka mikakati ya kuwezesha mazingira bora kwa sekta ya mauzo ya nje ya nchi (EPZ, ripoti ya hivi majuuzi ikionyesha kuwa taifa linaendelea kuvutia wawekezezaji katika sekta hiyo. Hata hivyo serikali kuu inategemea  hiyo na ile ya kibinafsi kuunda nafasi za kazi kwa vijana na kukuza mauzo ya nje ya nchi […]

MARUFUKU YA MAHAKAMA KWA POLISI

Jaji wa Mahakama kuu Mugure Thande amewapiga marufuku maafisa wa polisi dhidi ya kutumia malori ya kurusha maji, vitoza machozi, risasi za chuma na zile za mipira au silaha zozote butu dhidi ya wanaofanya maandamano ya amani kupinga mswada wa fedha ambao umetupiliwa mbali. Katika kesi iliyowasilishwa mahakamani humo na mkenya kwa jina Saitabao Ole […]

PETER AGORO AELEKEA MAHAKAMANI KUTAKA BARAZA LA VIJANA LA KITAIFA KUFANYA UCHAGUZI

Ombi limewasilishwa kutaka kulazimisha Baraza la Kitaifa la Vijana kufanya uchaguzi wa wawakilishi wa vijana kama ilivyoainishwa katika katiba. Katika ombi lake, Peter Agoro anahoji kuwa baraza hilo lilianzishwa ili kuwakilisha masilahi ya vijana nchini Kenya, kuwezesha ushiriki wao katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa nchini. Agoro anasema kuwa kushindwa kufanya uchaguzi unaohitajika kumesababisha […]

WASALITI NAMBA MOJA; LSK WAAMBIA WABUNGE

Chama cha wanasheria nchini LSK kimewasuta wabunge wa bunge la kitaifa kwa madai kwamba wamewafeli wakenya. Kwa mujibu wa rais wa LSK Faith Odhiambo wabunge wamekuwa wakitumika kutimiza ajenda za serikali badala ya kutimiza agenda za mwananchi mpiga kura. Odhiambo vile vile ametumia fursa hiyo kuwasuta viongozi na serikali kwa jumla kwa kupelekea wakosa kukosa […]