BUNGE LA BUNGOMA LAWACHUNGUZA MAWAZIRI WAWILI

Wawakilishi Wadi katika bunge la Kaunti ya Bungoma wakiongozwa na kiongozi wa walio wengi Juma Nyongesa, wameapa kuendeleza uchunguzi dhidi ya Waziri wa Fedha Chrispinus Barasa na Waziri wa Elimu kwenye kaunti nhiyo Benedict Emachar kuhusiana na madai ya matumizi mabaya ya fedha za basari na ‘ufadhili wa kaunti maarufu kama Scholarship ya mwaka wa 2023/2024
Akizungumza baada ya kikao cha kuwahoji wawili hawa waliofika mbele ya bunge hilo kujibu maswali kuhusu matumizi ya fedha hizo, Nyongesa amesema wawili hao wameshindwa kujieleza, na kuahidi kwamba watawajibishwa kisheria.
Aidha, amesema idadi kubwa ya wanafunzi wamekatiza masomo yao kutokana na ukosefu wa karo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa