#Local News

POLISI WALAUMIANA KUHUSU MAUAJI

Idara ya upelelezi DCI imejitenga na mauaji ya bloga Albert Ojwang licha ya kukamatwa na maafisa wa idara hiyo, mkurugenzi mkuu wa DCI Mohammed Amin akitaka OCS wa kituo cha polisi cha Central Samson Taalam kuchukuliwa kama mshukiwa mkuu wa mauaji hayo.

Akiwa mbele ya seneti, Amin ametilia shaka hatua ya Taalam kudinda kumwandikisha Ojwang kwenye kitabu cha matukio yaani OB alipowasilishwa kituoni humo, akisema huenda kuna maelezo fiche aliyoyafahamu.

Hata hivyo, Taalam amesema kuwa Ojwang aliwasilishwa kituoni humo akiwa katika hali mbaya na kwamba wakuu wa usalama wanalenga kumtumia katika tukio hilo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *