MUSINGU YAPATA PIGO KWA KUPATIKANA NA HATIA
Timu ya soka ya Shule ya upili ya wavulana ya Musingu High imepata pigo baada ya kupatikana na hatia ya kuwachezesha wanafunzi wasiofaa kisheria na kubanduliwa kutoka kwa michezo hiyo.
Hii ni baada ya mahasimu wao Kakamega High kuwasilisha kesi ya rufaa dhidi yao wakidai Musingu walitumia Wachezaji ambao wamepitisha umri hitajika wa Wachezaji wasiozidi Miaka 19 kushiriki mechi baina ya shule za upili humu nchini.
Kwenye rufaa hiyo Kakamega High walidai Wachezaji wawili wa Musingu walikuwa wamepitisha umri kwa hivyo walicheza dhidi yao kinyume na sheria.
Sasa Kakamega High pamoja na Butere Boys zitawakilisha kaunti ya kakamega kwenye michuano ya eneo la magharibi kuanzia Leo hii mjini mumias.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































