JUNIOR STARLETS WAREJEA BAADA YA MICHEZO YA KIRAFIKI

Timu Ya Wasichana Ya U17 Ya Kenya, Junior Starlets, Ilimaliza Ziara Yake Ya Morocco Kwa Ushindi Wa 2-0 Dhidi Ya Morocco U17, Kufuatia Sare Ya 1-1 Katika Mechi Yao Ya Awali Ya Kirafiki.
Elizabeth Ochaka Alifunga Katika Mechi Zote Mbili, Huku Mitshel Waithera Akifunga Pia Katika Mchezo Wa Pili.
Ziara Hiyo Ilitoa Mwangaza Muhimu Kabla Ya Mechi Yao Ya Mwisho Ya Kufuzu Kwa Kombe La Dunia La Fifa La Wanawake U17 2025 Dhidi Ya Cameroon. Mechi Ya Kwanza Itachezwa Aprili 20 Kwenye Uwanja Wa Nyayo, Na Marudiano Aprili 25 Huko Yaoundé.
Mshindi Wa Jumla Atafuzu Kwa Kombe La Dunia, Linalopangwa Oktoba 17–Novemba 8 Nchini Morocco.
Junior Starlets Sasa Wanalenga Kuweka Historia Kwa Kufuzu Kwa Makala Mbili Mfululizo Za Kombe La Dunia.
Kwengineko Timu Ya Wakubwa Harambee Starlets Ilichapwa Mabao 2-0 Na Wenyeji Wao Ivory Coast Kama Ilivyotokeo Kwenye Mechi Yao Ya Kwanza Ijumaa Iliyopita Katika Uga Wa Félix Houphouët-Boigny Mjini Abidjan.
Kenya Walitumia Mechi Hizo Kujipima Kabla Ya Mechi Ya Kuwania Kufuzu Kwa Wafcon Dhidi Ya Gambia Mwezi Oktoba.
Kulingana Na Viwango Vya Fifa, Ivory Coast, Ambao Walicheza Kombe La Dunia Kwa Mara Ya Kwanza Mwaka Wa 2015, Wako Katika Nafasi Ya 71 Duniani, Ambayo Ni Nafasi 71 Juu Ya Kenya Iliyo Katika Nafasi Ya 142.
Imetayarishwa na Nelson Andati