‘SERIKALI YANGU IMESIMAMISHWA NA MAOMBI’ RUTO ASEMA

Rais William Ruto amewashauri wakenya mkujendelea kufanya kipaumbele maombi akisema kuwa yatasaidia kuimarisha taifa hili kwa kulainisha mambo mbali mbali
Akitoa hotuba yake katika hafla ya maombi ya kitaifa ambayo yanaendelea kwa sasa katika hoteli ya safari Park rasi anasema tangu achukue hatamu za uongozi mwaka wa 2022 serikali hyake imesimamishwa na maombi
Kwa mujibu war ais juhudi zinazowekwa na serikali zinaambatana na maombi na ndiposa matokeo yake huwa kamilifu
Amepeana mfano wa mvua iliyonyesha baada ya kiangazi kikubwa ,utoshelezi wa chakula na kuyalipa madeni
Kauli ya rais Ruto imetiliwa mkazo na naibu wake Rigathi Gachagua akisema kuwa serikali ya kenya kwanza itazidi kupiga hatua za mbele kutokana na msingi wake kimaombi
Imetayarishwa na Janice Marete