VILABU VIJIPANGE UPYA
Kuahirishwa kwa mwanzo wa msimu wa ligi ya kitaifa ya daraja la pili soka ya wanaume NSL ni baraka kwa kuwa kutasaidia vilabu kufuata sheria mpya za CAF, huu sio usemi wangu bali wa kocha wa Luanda Villa Gilbert Selebwa.
Msimu wa NSL 2024/25 utaanza Septemba 21 baada ya kuahirishwa kwa wiki mbili na Shirikisho la Soka la Kenya.
Hata hivyo, anahisi kucheleweshwa huko kutaathiri vilabu vilivyotumia pesa kwa maandalizi ya mapema.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































