RAILA AJIPIGIA DEBE KUWA MWENYEKITI WA AU HUKO ZANZIBAR
Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga ameendeleza kampeni za kuwania wadhifa wa mwenyekiti wa umoja wa africa AU huko Zanzibar ambapo alihudhuria kongamano la mawaziri wa jumuiya ya afrika mashariki.
Akizungumza katika kongamano hilo Odinga amesema kuwa afrika ina nafasi nyingi sana za kujiimarisha kiuchumi na vile vile kujiendeleza kama bara huku akishinikiza kupanuliwa kwa mbinu za usafiri kupitia anga ,barabara na bahari ili kufungua mipaka ambayo kwa sasa inawazuia waafrika kutangamana inavyostahili.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































