TAIFA LAUGUA SERIKALI, UPINZANI WAKILAUMIANA
Wakenya wameachwa gizani kuhusu lengo na wahusika wa mauaji na uharibifu wa mali wakati wa maandamano, serikali na upinzani zikiendelea kurushiana lawama bila kukubali kuwajibika.
Kulingana na Rais William Ruto, upinzani una njama ya kuipindua serikali, akiapa kwamba kamwe serikali yake haitaruhusu jaribio hilo kufanyika.
Hata hivyo, mrengo wa upinzani ukiongozwa na aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua umepinga madai hayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































