#Local News

MAHAKAMA ELDORET KUMHUKUMU ALIYEKIRI KUWAUA WATOTO 5

Mahakama kuu ya Eldoret imeratibiwa kutoa hukumu hapo kesho dhidi ya Evans Juma Wanjala, mshtakiwa aliyekiri kutekeleza mauaji dhidi ya watoto 5 katika eneo la Moi’s Bridge kaunti ya Uasin Gishu.

Hii ni baada ya jaji Reuben Nyakundi kumpata na hatia ya kutekeleza unyama huo dhidi ya watoto hao wa kati ya umri wa miaka 10 na 15, Nyakundi akitegemea stakabadhi za matibabu na ripoti ya DCI kutoa uamuzi huo.

Miongoni mwa waliouawa ni Stacy Nabiso mwenye umri wa miaka 10, ambaye mshtakiwa aliwaambia maafisa wa DCI kuwa alimnajisi kabla ya kumnyonga hadi kufa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAHAKAMA ELDORET KUMHUKUMU ALIYEKIRI KUWAUA WATOTO 5

BLOGA NDIANG’UI APATIKANA

MAHAKAMA ELDORET KUMHUKUMU ALIYEKIRI KUWAUA WATOTO 5

NITABADILISHA AFC ASEMA AMBANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *