#Local News

SERIKALI YA HOMA BAY KUJENGA MADARASA 160 YA ECD

Serikali ya kaunti ya Homa Bay inakusudia kujenga madarasa 160 zaidi ya elimu ya awali ECDE kama sehemu ya mkakati wa matokeo ya haraka.

Mpango huo, Madarasa ya Genowa Ondoa Kaunda, ulianza katika Shule ya Msingi ya God Ndonyo katika kata ya Kibiri, eneo bunge la Karachuonyo siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

Gavana Gladys Wanga amesema mpango huo, ni sehemu ya jukwaa lake la kampeni, utafaidi kata zote 40 kwa usawa, na kutoa kila moja idadi sawa ya madarasa.

Uongozi uliopita ulijenga madarasa 20, huku mengine 33 yakikwama katikati.

Kila darasa litagharimu Shilingi milioni 1 huku fedha hizo zikidhibitiwa na shule na jamii ya eneo hilo.

Imetayarishwa na Janice Marete

SERIKALI YA HOMA BAY KUJENGA MADARASA 160 YA ECD

AJIUA BAADA YA KUUA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *