JUHUDI ZA SADC, EAC KUREJESHA UTULIVU DRC
Huenda machafuko yaliyo mashariki mwa taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC yakakomeshwa na utulivu kurejea nchini humo, kufuatia pendekezo la mazungumzo baina ya serikali ya DRC na wapiganaji wa M23.
Kwa mujibu wa Rais William Ruto ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuna haja ya hatua za dharura kuchukuliwa ili kusitisha mapigano hayo ambayo yamesababisha vifo na mamia ya familia kupoteza makazi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































